NILIUZWA KUWA MTUMWA WA BILIONEA 12 "Ni kama hujafurahia Mimi kuwa hapa...." Jessa aliongea
"Unaelewa nini kuhusu neno Mtumwa
"Sidhani kama kuna haja ya Mimi kukuelezea,"
"Nitakueleza kwa ufupi, Mtumwa ni mtu asiye na uhuru. Kama utakaa hapa hautakuwa na uhuru nata....." Kabla Ciara hajamaliza maneno yake Jessa alimkumbatia
"Usimlaumu Mama katika hili, tamaa yangu ya kutaka kukuona ndio imefanya nije hapa"
"Nakupenda mdogo wangu..... nitatafuta namna ya sisi kuwa Watumwa huru" Ciara aliongea
Basi kwa pamoja walitoka nje, Katy akiwa juu ya kibaraza alimshuhudia Jessa.
Moyo wake ulilipuka, tangu azaliwe hajawahi kuona msichana mrembo kama Jessa.
Taratibu alishuka kwenye ngazi mpaka akawafikia
"Naomba unifuate....." Katy alimuamrisha Jessa
"Ni Mama yake Mike hutakiwi kumbishia ...." Ciara aliongea
"Huyu si jeuri kama wewe hata kama nisingekuwa Mama yake Mike angetii amri yangu" Katy aliongea
Ciara hakuwa na kitu cha kuongea, alimuacha Jessa aondoke na Katy
"Wee Mtumwa wa kiume hebu njoo hapa... " Katy alipaza sauti
Basi Mtumwa alikuja kwa kukimbia nusu adondoke
"Mbebe huyu Msichana"
"Yaani unataka ni mbebe Mtumwa mgongoni"
Katy hakujibu chochote badala yake alimtazama Mtumwa wa kiume kwa jicho baya
Mtumwa huyu aliingiwa na hofu, bila kupoteza muda aliinamisha mgongo wake akambeba.
"Napelekwa wapi mie...." Jessa alijiuliza huku mapigo ya moyo wake yakidunda
Baada ya kufikishwa ndani Katy alitoa amri Jessa aogeshwe
"Kwanini mnanifanyia hivi...." Jessa alijikuta akiuliza baada ya kuona haelewi
Unastahili kuwa Mke wa Mike na si kuwa Mtumwa kwenye nyumba hii. Tangu ni zaliwe sijawahi kuona Binti Mrembo kama wewe, umeweza kuuendesha moyo wangu kwa haraka sana naamini hata kwa Mike itakuwa hivyo" Katy aliongea
"Unataka niolewe na Bilionea Mike?" Jessa aliuliza kwa mshangao
"Acha papara, endapo utafuatisha nini nataka kila kitu kitaenda sawa...." Katy aliongea
Basi Jessa alivalishwa mavazi ya gharama kubwa sana kiasi kwamba Watumwa wote walishtuka
"Ana sura ya kuvutia lakini hana vigezo vya kumvutia Mike...." Mtumwa Jala aliongea
"Una maanisha nini kusema hivyo" Watumwa wote waliuliza kipamoja
"Ciara ndio atakuwa mke wa Mike ni suala la muda tu" Jala aliongea
Watumwa wote walikaa kimya tu basi kama kumheshimu lakini kwa jinsi Jessa anavyo vutia waliamini yeye ndio atakuwa mke
Mida ya jioni Mike alielekea chumbani kwa Ciara kama kawaida yake.
Siku ya leo alikuwa anajisikia kukaa bustanini hivyo wote kwa pamoja walikaa wakaanza kutazama nyota za angani
"Tangu ni kuambie nakupenda hukuwahi kunijibu.... naomba kusikia kutoka kwako siku ya leo" Mike aliongea
"Nipe muda nizitafakari hisia zangu vyema.....na hata hivyo Mimi ni Mtumwa wako huna haja ya kuniuliza hivi"
Mike alipuuzia jibu alilopatiwa kwa kumpiga busu lililobeba hisia kali
"Samahani kwa kuwa vurugia...." Sauti ya Katy iliwashtua
Siyo Mike wala Ciara hakuna aliyeonesha kushtuka, ni wazi wote wameota sugu hawakuwa wakimuogopa
"Nimevutiwa na Mtumwa uliyemnunua leo naomba umuache awe mali yangu....kuna namna natam..." Kabla hata Katy hajamaliza maneno yake Mike alimkatisha
"Mchukue na umfanye vyovyote vile unavyotaka"
"Ahsante kwa kuwa muelewa...." Katy aliongea kisha akaondoka, alipiga hatua kumi kisha akageuka nyuma.
Alistaajabu kuona Mike akimbusu Ciara.
"Sielewi huyo binti ana nini lakini ni suala la muda tu Jessa atanizalia wajukuu wazuri" Katy alijisemea kisha akaendelea na safari
Jessa hakupata nafasi ya kulala, Katy alikuwa bize kumfundisha namna ya kuvaa, kujipamba na kula kidada zaidi.
Kadri siku zilivyoenda ukaribu kati yao ulijengeka na hata Jessa akasahau kabisa kuhusu Mama yake.
Alianza kumuona Katy kama Mama yake. Kuna muda hata waliweza kucheza michezo ya kitoto
Ciara alifurahi sana kwa namna Katy alivyokuwa anampenda Jessa
"Uzuri wake umembeba...." Ciara alijisemea ndani ya moyo wake kisha akaendelea na safari yake
Itaendelea π₯
Full 1000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni