๐บ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 165 - 172
165
Tulicheka pamoja huku tunalia sana mpaka simu ikakata.
Joan aliniinua pale chini na kunikumbatia. Alinikumbatia na kuniambia โuliniambia nisilie nimumini Mungu, niombe kwa nguvu, ulinifuta machozi Ndeana. Sitaki kuamini wewe ni mdhaifu namna hii. Kwasasa wewe unatakiwa sana kusimama kidete kutetea penzi lako. Kuwa makini sana, muombe Mungu na msaidie mwenzako.
Sikia Stewart ni Tajiri, ana watu wenye pesa. Anajua apite wapi na wapi apite kufikia malengo. Anaumia kwasababu kapoteza ila hawezi poteza milele. Na hata hivyo pengine tayari ana mipango anataka tu wewe ndiyo upambane kufikia ndoto zake yaani umsaidie kwa mawazo, umpe utulivu na vitu kama hivyo. Kuwa imara ndugu yangu.โ
Nilimtazama Joan nakusema โhapa kazini, kila mmoja ananicheka, ananikejeli nitaishi vipi sasa.โ
Alitabasamu na kusema โNdeana kimya chako kinakusaidia sana. Wewe ni mwingi wa Hekima. Kwakuwa unajua nini unataka fanya kazi. Fanya kazi achana nao. Hawa wote wapo hapa kipesa tu usihangaike nao hata mara moja.โ
Sikuweza hata kutabasamu kwakweli, niliendelea tu kufuta machozi na kisha aliniambia โtwende tukaendelee na kazi na baada ya hapo uwahi kwa mwenzio.โ
Nikatabasamu kwa mbali nikiwa hoi.
Baada ya hapo taratibu tulishikana mikono kutembea kuelekea ndani. Tulifika mpaka ndani, na kuanza kazi. Nafanya kazi huku ukiona wadada wahudumu ni kumsema Boss. Yaani ilikuwa ni ngumu sana kwangu, kila wakipata nafasi unaona kabisa wananicheka. Mmoja nilisikia akisema โalikuwa anaringa huyu, kidogo tu amepandisha huko juu. Haya tutaona sasa.โ
Nilimtazama tu na kuendelea na kazi. Sio kama hapakuwa na watu kama Joan, ila ni wachache sio kama wanaonicheka na sasa siamini naona kama wananikejeli tu.
Nilikuwa nikipata muda kidogo wa kuwa mwenyewe ninajificha na kulia, nalia kisha narudi naendelea na kazi. Ni siku ambayo ilikuwa mpya, hadithi ni Boss mpya tu. Boss wa zamani amesahaulika tayari. Roho iliniuma sana, roho ilikuwa inawaka moto kwa maumivu makali sana.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 166
Nilifika sehemu ya kubadili nguo muda ulipofika. Basi nikabadili nguo huku naumia sana. Nilikutana na ujumbe wa baby wangu Stewart, alikuwa ameandika โMy sweet Person Are you Ouk?โ
Nilitabasamu kidogo nikiwa na unyonge nilimjibu โbaby nipo sawa, naomba kukuona kipenzi.โ
Alinijibu haraka haraka โnakusubiri kwa hamu Ndeana wangu, nakusubiri.โ Kisha alinipa maelekezo.
Nikamjibu โNakuja, nakuja sio muda mrefu.โ
Akaniambia kuwa ananisubiri kwa hamu sana. Unajua namna tunavyowasiliana, vitu vimekaa kinyonge sana.
Basi mimi nikatoka taratibu, wakati natoka nimefika getini nashangaa sijui hata nishike njia gani. Joan alitoka na aliniambia โrafiki yangu upo sawa?โ
Akatoka mdada kwa nyuma akisema huku anacheka โatakuaje sawa.โ
Nilimtazama tu na kuyazuia machozi yangu.
Joan aliniuliza tena โunaenda wapi kwani?โ
Nikamwambia, akanijibu akisema โtwende mimi naishi kituo cha mbele ya hapo. Haya twende tuongozane.โ
Tuliungana mini na Joan, mpaka sehemu ya kupata usafiri. Tukapanda daladala na safari ilianza. Ninakumbuka sana, namna nilikaa kimya kwenye gari siwezi kuzungumza kitu, yaani nimetulia tuli. Mpaka nimefika tu hicho kituo Joan ndiyo kaniambia na ndiyo nikashuka.
Niliposhuka nikachukua simu yangu na nikampigia Boss wangu, yaani Stewart. Aliniambia โPole kipenzi, changu.โ
Nikamwambia โAsante baby.โ
Basi alinielekeza niulize kwa mtu gani hivi na vile nami nikafuata mpaka nikafika. Nilifika sehemu aliyonielekeza. Sio nyumba mbaya wala sio nzuri. Nzuri tu kawaida inafaa kuishj watu. Nilibisha hodi, na haraka mlango ulifunguliwa.
Mlango ulipofunguliwa kwanza tulianza kutazamana huku nikiita โStewart!!!โ
Machozi yakashuka, na yeye pia machozi yakashuka akiita โNdeana!!!โ
Kisha alinikumbatia kwa nguvu sana pale mlangoni. Nilijisikia uchungu mno kumuona mwanaume wangu kwenye ile hali. Pamoja tulijikuta tunalia kwa uchungu. Tulilia tena sana huku tukiingia ndani. Tulilia mno, tena nililia nikisema โkwanini uliumia peke yako na hukunitafuta mimi, kwanini?โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 167
Stewart alilia akisema โnisamehe totoo, nilichanganyikiwa sana. Ndeana heshima ya mwanaume ni kazi. Kila nilipokuwa nawaza nitaishi bila kazi nilikuwa nazidi kuchanganyikiwa natumai unanielewa mpenzi. Nisamehe sana.โ
Alinifuta machozi akiniambia โNdeana inatosha, tumelia sana. Sio vizuri tutaumwa. Sikianikuambie kitu kipenzi. Najua tutapitia wakati mgumu sana. Ila mambo yatakaa sawa. Nitajitahidi sana. Najua wameshikilia mpaka akaunti zangu. Ila nitafuatilia. Tutateseka mwanzo tu ila yatakaa sawa si unaniamini totoo.โ
Nikasema โNakuamini sana. Na pia ninakupenda sana. Stewart wametambulisha Boss mpya!!โ
Alinitazama na kusema kwa huzuni โlazima wafanye hivyo. Hawawezi kukaa bila kiongozi. Ndeana kila kitu duniani ni cha kupita tu. Nimejifunza kuwa natakiwa kupambana zaidi ya mwanzo. Jambo hili kama mwanaume linaniumiza sana.
Ila ninayi imani, ninaamini nitashinda hii vita sijui ni lini ila nitapita tu. Nina hofu moja tu, kukupoteza wewe, hii itanifanya nishindwe kuendelea kabisa, unajua tangu nimekufahamu maisha yangu yanakutegemea sana.โ
Nilitabasamu ba kusema โUnahisi nitaweza kuishi bila wewe?, siwezi wala huwezi kunipoteza baby wangu. Mimi na wewe tupo sambamba. Ulipo nipo. Nakupenda sana.โ
Akanikumbatia na kusema โNAKUPENDA.โ
Nami nikajibu โNAKUPENDA.โ
Tulipeana busu, na kutabasamu kidogo walau hali ile ya uchungu ilikuwa inapungua.
Kiuhalisia ni kuwa mwanaume huyu, alikuwa katikati ya maumivu. Hata ile sura yake ya tabasamu muda wote ilimuondoka. Alikuwa muda mwingi anazubaa kama vile anawaza kitu. Nami namtazama na kuanza kumuongelesha kama vile โbaby rafiki yako yupo wapi?โ
Alinitazama kwa upole akanianbia โyupo kazini toto!!โ
Nikatabasamu tu na kusema โsawa kipenzi, au twende nyumbani?โ
Akacheka kidogo na kusema โkipenzi, najua utatamani kila kitu kiwe sawa. Ila mimi na wewe ni wapenzi tu bado sijafanya lolote kwako. Sio heshima mimi kuja kwenu. Nipo sawa kuwa hapa.โ
Nikamtazama na kusema โnina njaa leo sijala siku nzima, wewe umekula baby?โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 168
Alinitazama tu. Nikajua tu hajala. Ilinibidi kwa pesa yangu nifanye maarifa. Nikatoka nje na kuuliza sehemu naweza kupata mahitaji hayo. Nikaelekezwa na huyo mdada jirani.
Akampigia simu kijana wake wa pikipiki na tukamuagiza hivyo vitu kisha nikarudi ndani kusubiri na nilikaa kwa muda kidogo kisha nikaitwa nami nikatoka na pesa nikalipia na kurudi ndani.
Nilipika na kwa pamoja tulikula ingawa kivivu sana. Tulipomaliza Stewart alikuwa ananitazama tu usoni. Kisha alitabasamu na kuniambia โNdeana, wewe ni mwanamke ambaye kila mwanaume mwenye utimamu anatamani kuwa naye. Una upendo, utu, heshima, adabu, na unapenda sana furaha. Tazama namna unahakikisha nakuwa sawa hata katikati ya machozi umekuwa furaha yangu. Ndeana ninakuamini sana, kuliko kitu chochote kile. Ninakuamini kuliko kwasababu silaha kubwa ya mapenzi ni uaminifu.โ
Nilitabasamu nikisema โwewe ni mwanaume mzuri sana, sipendi kuona ukiwa na huzuni. Ninakuombea heri, mafanio, furaha, upendo na amani.โ
Akatabasamu tu kisha aliniambia โunaweza, unaweza kulala hapa leo?, samahani lakini ila nahitaji mtu wa kuwa naye.โ
Nikamwambia kwa kutoa macho โmwenzio hatochukia?โ
Alinitazama akisema โana kufahamu sana, wewe ndiyo umfahamu.โ
Nikacheka tu, basi nikamwambia โnitaongea ma baba, si unajua dada naye siku hizi hatulii nyumbani. Kama kutakuwa na lolote basi nitakwenda akikubali nibaki basi nitabaki.โ
Alitabasamu na aliniambia โumependeza sana, una rangi nzuri sana. โ
Nikatabasamu.
Basi niliwasiliana na familia yangu, watasema nini juu ya Stewart. Wanavyompenda na kumuamini. Baba yangu alitaka kujua kuhusu maendeleo ya Stewart na mimi nikamwambia kuwa tutaongea pale nitakaporudi nyumbani. Hivyo siku hii mimi nilibaki hapa.
Stewart anapenda movie, basi nilikaa katikati ya mapaja yake ule usiku. Tukawa tunaangalia movie. Tuliangalia movie nzuri sana ilikuwa inaendana na hali yetu tunayopitia.
Kuna mahali mpaka tunaacha movie tunalia kweli. Kwingine tunacheka na kutabasamu. Basi tuliendelea hivyo mpaka rafiki yake akarudi. Aliponiona alisema โooh shem upo hapa. Karibu sana.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 169
Nilisema kwa upole โnashukuru sana.โ
Kitu cha kwanza alisema โnimeleta chakula, mmekula?โ
Stewart akasema โnilisahau kabisa kukupigia. Shemeji yako amepika.โ
Akasema โbasi tena hizi chips hazitushindi na chakula tutakula.โ
Tukacheka tu. Lakini ukitazama Stewart hana raha kabisa ni mtu tu wa kuhuzunika. Kiasi huyu rafiki yake alisema โRafiki yangu Stewart, huwezi kuwa hivyo kila siku, huwezi kuwa hivi kabisa. Ninakuomba sana usiwaze. Hata mimi niliwahi kupitia haya mapito.
Sikuwa na kazi wala sikuwa na pa kulala. Ila Mungu alinipigania. Muhimu kwasasa ni muongeze upendo, muongeze imani mpendane sana. Mimi nipo pamoja na wewe mpaka utakapokuwa sawa.
Nakuomba sana Stewart, usimpe msongo shem. Nadhani yeye anapitia wakati mgumu zaidi kwa maana bado kabaki kazini. Msimpe shetani nafasi nawaomba sana.โ
Stewart alivuta pumzi na kusema โninakuonea huruma sana Ndeana. Unajua kaka nakuelewa vizuri sana. Ila nawaza nitaishi vipi. Kila nikiwaza nguvu zinaisha. Mwanamke wangu, mwanamke wangu nampenda sana. Natamani nimpe kila kitu ila sitaweza. Najua ataumia sana, nami sitaki kumuumiza.โ
Shem alinitazama na kusema โshem, mchukue, nendeni chumba kile pale. Mwenzako anahitaji kupumzika sana . Hayupo sawa bado. Anakuhitaji mno.โ
Nilimtazama Shem na kusema โAsante Shem, usiku mwema.โ
Basi nikamuinua na tukaenda chumbani. Kufika chumbani alijitupa tu kitandani. Nilimuonea huruma sana. Yeye alinitazama na kusema โNjoo kipenzi, njoo nikukumbatie.โ
Nami nilienda pale, kwaajili ya kufanya hivyo.
Tulijikuta tumelala tumekumbatiana tu mpaka asubuhi mimi ndiyo niliwahi ili niende kazini. Na nilijiandaa, nikamfanya na yeye aamke. Tulisalimiana kwa busu kama kawaida yetu na niliagana naye. Nakumbuka aliniambia โFanya kazi kwa bidii. Kuwa makini mrembo wangu. Ninakupenda sana. Ninakupenda kuliko kitu kingine chochote.โ
Nikatabasamu na kumpa busu nikisema โchangamka basi baby, Nakupenda zaidi My sweet person.โ
Akatabasamu.
Nilienda mpaka kituo cha daladala, nikapanda gari na kuanza safari. Siku hii kazini nilikuta Joan kafika. Aliponiona sijabadili nguo alitabasamu na kuniuliza โBoss anaendeleaje?โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 170
Nikatabasamu na kusema โanaendelea vizuri sana. Ila najua anajikaza tu. Ukiona macho yake yamejaa huzuni nami nataka kumsaidia.โ
Rafiki yangu aliniambia โhata ningekuwa mimi nisingekuwa sawa. Ila Unatakiwa wewe ujiongeze. Mshahara wa hapa, mahitaji yako na umsaidie na mwenzako hapana haitoshi. Mimi huwa napost na vyombo vya nyumbani mtandaoni. Watu wanazoea sana. Na nauza japo sio sana ila nauza.โ
Nilitabasamu nikisema โunafikiri nitaweza?โ
Akaniambia โsubiri nakutumia hapa saizi wewe post tu. Hata wasiponunua siku watanunua tu.โ
Nikatabasamu, huku ananitumia mimi moyoni nasema napost tu ila sio mambo yangu.
Basi Joan aliniambia โKipenzi, baba mtoto alinitafuta sikuamini. Kweli Mungu ni wa ajabu sana. Huwezi amini, kalipa mpaka kodi ya nyumba na kasema kila mwisho wa mwezi atanipa pesa ya matumizi.โ
Nikasema โweee usiniambie?โ
Joan alisema โnaona mwanga kidogo, nashukuru rafiki yangu. Nashukuru sana.โ
Tulikumbatiana. Kisha nikamaliza huko kupost na kuweka simu zetu mahali huwa tunaweka.
Kitu nilikuwa siwezi kuzuia ni kuchekwa kazini, watu kunidhihaki na vitu kama hivyo. Sikuwa naweza kuvumilia. Ndiyo kwanza siku ya pili ila nipo hoi kwa kuchekwa. Nachekwa sana. Ninachekwa roho inaniuma ila nitafanya nini sasa.Zaidi ya kulia na kuumia.
Muda wa kutoka ulifika. Simu yangu nimezoea nilikuwa nawekewa bundle la mwezi sasa nalo limeisha wakati mbaya. Hivyo nikasema nikifika nyumbani nitanunua.
Basi nikaanza safari ya kurudi nyumbani. Nilikuwa nachelewa sasa kwasababu usafiri ni wa shida ila sina namna. Nimefika tu dada kanipokea, โmdogo wangu imekuaje huko, amefanikiwa?โ
Nilitikisa tu kichwa huku machozi yanatoka. Nilisema โkila kitu kimeisha, anaumia sana, analia sana.โ
Dada alinikumbatia akisema โhakuna jaribu lisilo na mlango. Hakuna Dua isofika kwa Mungu mdogo wangu. Kuwa na imani.โ
Nilimtazama dada na kusema kwa uchungu โkazini dada, kaletwa boss mpya. Wafanyakazi wananicheka sana, sina raha wananitania na kunicheka wakati wote. Nitafanya nini sasa.โ
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 171
Dada alisema โAchana nao wewe angalia mahitaji yako na upige kazi. Acha wakucheke tu itafika muda watazoea.โ
Nlilia nikisema โdada natamani hata kuacha
kazi.โ
Dada alisema kwa kushangaa โunachanganyikiwa?, mwenzio hana kazi na wewe uache una wazimu wewe.โ
Nikalia tu na dada alisema โkaa imara, fanya kazi mdogo wangu. Acha wacheke, watanie na kukudhihaki ni hayo ni mambo ya muda tu. Yanapita kama upepo. Na vipi yeye anaishi wapi sasa?โ
Nikamuelezea dada yangu. Nakumbuka dada alisema โmaskini shemeji yangu, mkarimu sana. Ila ninamuamini sana. Mungu atamsaidia tu.โ
Baba alitoka chumbani na alitukuta tunalia. Akauliza โwanangu kuna taarifa gani?โ
Dada akaelezea na baba alisema โMungu wangu!!, sasa nitaishi vipi mimi, ina maana Mungu hakuangalia hili kuwa namtegemea. Dawa zangu mimi.โ
Dada alimtazama baba na kisha baba alisema โMungu hakupi jaribu usiloliweza. Tutavuka tu kwa hili.Wanangu, msilie, Ndeana. Simama na mwenzako iwe shida iwe raha. Mungu aliyemuinua mwanzo atamuinua tena na tena. Hivyo nenda kapumzike hakuna kulia.โ
Baada ya kufika chumbani, Stewart alinipigia, nikapokea na yeye aliniambia โtotoo, usiniambie ulikuwa unalia?
Nikafuta machozi na kusema โhapana niko sawa tu. Umeshindaje mpenzi wangu.โ
Aliniambia โNakumiss kila muda Ndeana wangu.โ
Nikatabasamu na kusema โAsante sana Stewart, hata mimi nakumiss mno.โ
Aliniambia kwa upole โhabari za kazini mke wangu.โ
Nikatabasamu machozi yakitoka. Sikuwa nataka kumuumiza. Nilisema tu โnipo sawa kabisa. Kazi tu zimekuwa nyingi sana.Ila nishazoea sasa si unajua.โ
Alitabasamu na kusema โNi ngumu ila namiss kila kitu, unajua kukaa tu nyumbani inaumiza nawaza ningekuwa nakuona na sare zako ukihudumia, ukija ofisini kwangu. Ndeana inaniuma.โ
Nikatokwa na chozi nikisema โtumesema hatulii tena inatosha.โ
Na yeye aliniambia โkweli hatulii tena.โ
Nikamwambia โI love you Stewart!!โ
Na yeye aliniambia โI love you more than the word itself. Nakupenda My sweet Person.โ
Nikatabasamu tu. Na kisha aliniambia, Pumzika usiache kunitafuta.
๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐๐: 172
Nikacheka nikisema โnaanzaje?โ
Akaniambia โkama nikufuate vile, ila nikiwaza mpaka nianze kuhangaika na daladala nachoka.โ
Nikacheka nikisema โpole love, mimi nitafanya utaratibu nije tu wala usijali.โ
Kama masihara nikanunua bundle na kuwasha data. Nilikuta wateja watano wanataka vyombo tena vya gharama na ni wale wateja wangu huwa wananiachia namba na kuuliza mambo kadhaa pale hotel na mengine mengi.
Sikuamini nikampigia Joan. Joan alisema โnilikuambia wewe, sasa hapo waambie walipie. Kesho tukitoka kazini tunapita sokoni hapa na kariakoo karibu sana.
Nakupeleka kwa hayo maduka na leoleo nawaambia wakuweke kwenye magroup. Sikia kesho hiyohiyo unawasambazia tena wanakupa pesa ya usafiri. Kazi kwisha kazi. Una nyota hatari unajua hapo faida kubwa.โ
Nikacheka nikisema โMungu ni mwema, sasa nitapost kama mwenda wazimu. Nipate nikose nitapost tu siachi mimi.โ
Joan alicheka na kusema โumeweza haya sasa kesho rafiki yangu mimi kuna mahali nampelekea mteja.โ
Nakumbuka namna ambavyo niliwasiliana vizuri na mpenzi wangu. Alifurahia sana na vile nimemuelezea kuhusu biashara yangu. Akaniambia nitumie na mimi nikusaidie kupost. Nikamuuliza โwewe namba yako si ina watu wenye hadhi sana.โ
Alicheka na kusema โsasa mimi sina hadhi, itabidi wanunue tu vyombo. Mimi na mpenzi wangu tumeamua kuuza vyombo.โ
Nikacheka na kusema โBaby nakutumia kimoja tu kizuri, wewe utajua cha kuandika.โ
Akaniambia โni sawa kipenzi, ni sawa kabisa totoo muhimu upate wateja.โ
Nikacheka. Basi nikatuma na muda haukupita nikaona amepost kweli whatsp kaandika โ Kwa mahitaji ya vyombo vizuri na vya kisasa, support my sweet person, my Love.โ
Akaweka na namba basi akaniambia tusubiri.
Nilianza kupata Orders za vyombo mpaka siku inatofuata nilitamani nisiende kazini. Yaani huyu anasema nimeona kwa mwanaume wako, huyu anakuja wifi nipe hii, huyu anakuja madam naomba kama hii. Nilifurahi sana. Nilifurahi mno nami sasa nilijuta nilikuwa nachelewa wapi. Na hapo tunaambiana โwanakuja!!, baby watu wanakuja!โ
NAAAAAAAM HUU NDIO MWISHO WA SEASON YA NNE
SEASON YA MWISHO INATAPATIKANA WHATSAPP TU, KWA SH 1000
NO YA WHATSAPP NI 0743433005
KUMBUKA, SEASON FIVE AMBAYO NI YA MWISHO HAITARUSHWA HAPA FACEBOOK, KARIBUNI MJISOMEE WHATSAPP KWA BUKU (TSH1000)
๐ต๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐ฝ๐๐ ๐๐๐๐ ๐ด ๐๐๐๐ 0743433005 ๐๐๐๐ ๐จ๐ฎ๐ถ๐บ๐ป๐ฐ๐ต๐ถ
๐ผ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐พ๐๐๐๐๐จ๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ +255743433005 ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni