*AFANDE NILEGEZEE KAMBA ππ«π«* *14&15* Maneno ambayo Elijah alinambia yalinivunja moyo vibaya sana. Niliapa nikasema lazima nimulize Elton akirudi. Nilihitaji kujua sababu
yake ya kunibusu, maana matendo yake yote yalikuwa yanachanganya. Asubuhi ananipikia, ananijali, jioni anarudi anasema hanipendi Haikuniingia akilini
Basi Elton alirudi usiku sana kama saa saba usiku. Alipoingia ndani niliona kabisa amechoka na mood yake ni mbaya Lakini mimi sikujali
"wewe hujalala?β aliuliza kwa sauti ya ukali
"Nakusubin wewe, nataka kukuuliza kitu
"Kitu gani unataka kujua ambacho kinafanya usilale mpaka sasa ivi?"
"Mbona ulini-kiss asubuhi? Na mbona unajifanya unanijali wakati wewe mwenyewe unamwambia Elijah hunipendi? Unanichanganya. Nataka nijue hisia zako ni zipi hasal
Elton Alinitazama kwa sekunde chache kisha ghafla akaanza kucheka. Kicheko kile cha
dharau
"Hahaha wait...unajua wewe ni mjinga sana?
Kwa sababu tu niliku-kiss na kukujali kidogo ukadhani nakupenda? Una akili kweli? Wewe ni
tapeli tu Gina. Usiwaze mambo ya kipumbavu, Nilichokifanya ni kwa sababu ulikuwa mgonjwa, si kwa sababu nakupenda. Simple like that
Maneno yake yaliniingia kama kisu moyoni Nilihisi maumivu, machozi yakaanza kunitoka bila kujizuia. Nikamwangalia nikiwa nimeumia sana
"Kwa hiyo ulinichezea kwa sababu nilikuwa mgonjwa? Unajua hiyo imeniumiza kiasi gani? usingefanya kitu kama hicho kama ulikuwa unajua kabisa huna hisia na mimil
"Sorry kwa ilol Ukimaliza mwezi wako hapa, utarudi kuendelea na maisha yako. Sina muda wa mapenzi
Akageuka na kwenda zake chumbani, akaniacha nimesimama pale kama mtu aliyepigwa radi
Nilijiona mjinga, Nilijiona nimejidhalilisha kwa kumpenda mtu ambaye hana hata chembe ya hisia kwangu. Nililia muda mrefu, mwishoni
nikaenda kulala stoo kama kawaida Nikiwa huko bado nalla, mlango wa stoo
ukafunguliwa polepole, allikuwa ni Elijah. Allona nalia macho yamevimba mpaka akaumia kaka wa watu
"Actually nimesikia kila kitu na sijapenda alivyokuambia. So Gina really unampenda. Elton??"
"Ndiyo
"Elton hakufal Please chochote unachohisi kwake, futa. Kile alichokufanyia leo ni kuonyesha wazi kuwa hana time na wewe. Utakua unaumia
kila siku please
"Nimekoma Elijah! Haitajirudia tena
"Ok Sikiliza, usilale kwenye sakafu tena. Daktari alisema hutakiwi kulala kwenye baridi. Twende ukalale chumbani kwangu"
"Wewe utalala wapi sasa?"
"mimi nitalala kwenye kochi, Usiogope
Nilisita kidogo lakini alivyoniambia kwa upole nikakubali. "Sawa, asante"
Nilisimama kwa unyonge kama mfiwa, tukaongozana mpaka chumbani kwake. Alinipisha nilale kitandani yeye akajitupa kwenye zake kwenye kochi.
kitu
kilichotokea
hata
hatukuongeleshana maana kila mtu aligeukia upande wake. lle naishia tu usingizini, tukasikia mlango unagongwa kwa pupa kama vile anaegonga ana hasira kali. Nilishtuka,
Hakuna
Nikamwangalia Elijah kwa macho ya hofu. Nilijua lazima awe Elton
Ila wala hata Elijah hakushtuka, ndo kwanza Alisimama taratibu akaenda kufungua mlango. Alipofungua tu mlango, Elton akamsukuma
pembeni kisha akaingia ndani kwa nguvu akiwa
kavimba kwa hasira kama kifaru
Si Akaniona nimekaa kitandani nimejiachia??. Nyle nyle nilishtukia nashikwaa mkono kwa nguvu alafu navutwa kama gogo. Elijah alijaribu kumzuia ila alimshindwa Elton.
Elton ana nguvu sana ndo maana hakuona shida kunikokota na mkono mmoja. Ndani ya sekunde tano alishanifikisha chumbani kwake na mlango.
kaufunga kwa funguo nikasema Leo nauliwa
"Kwa sababu nimekukataa umeamua kwenda kwa Elijah? Unadhani mimi ni mjinga aliuliza kwa hasira
"Hapana Nilienda kwa sababu alinambia nisilale sakafuni
"Kwa hiyo hukuona chumba kingine chochote ila chake? Umekuwa kipofu ghafla sio?"
"Unanielewa vibaya! Hatujafanya chochote. Na kwanini una hasira? Ulinambia mwenyewe. hunipendi, sasa wivu wa nini?"
"Oooh so unadhani nina wivu??? Labda nikukumbushe kuwa unaishi hapa kama mfanyakazi wangu, kila kitu chako kinanihusu so Sitaki drama Ginah!"
Nikasimama nikisema "Mimi sina muda na wewe. Maneno yako yameniumiza sana leo. Please niache, sitaki mambo ya kipuuzi
Nilitaka kutoka chumbani kwake na nilikua nishaufikia kabisa mlango ndo nikakumbuka alifunga mlango na ufunguo
"Elton nifungulie mlango niondoke"
"Hakuna kuondoka.....please usiondoke" alisogea nyuma yangu akanikumbatia kwa
nguvu.
Alishusha pumzi kidogo akaendelea kuongea am sorry kama nilikuumiza. Nilikuwa na hasira, sikutakiwa kusema vile
"Sasa Kwanini uliniumiza hivyo?"
"Hasira zilikua za kazini Ginah! Na pia sikutaka kuonekana kuwa nakupenda but acha nikuambie ukweli. nakupenda
Nilishtuka, Moyo wangu ukaanza kudunda haraka. Sikudhani kama ningewal kabisa kusikia maneno hayo kutoka kwake.
Aliendelea kuongea akasema "Nilianza kukupenda siku ya kwanza tulipokutana pale club, Ila nilikasirika kwa maneno yako, nikajikuta
nakuchukia na kuapa lazima nikulipizie. But mbali ya kukufanya yote niliyokufanyia still bado nilikupendal Hujui ni jinsi gani nilivyokua nakosa
usingizi kila nilipo kuumiza au kukaripia then ukaribu wako na Elijah ukazidi kunichanganya kabisa! Mamaa mimi nina wivu sana tena mnol
So please usiendelee kuniumiza utaniua Ginah"
Weeeh Nikamkumbatia babaa kwa mahaba mazito, chezea penzi nini
"Nakupenda pia na nimekusamehe
"Kweli Ginah???"
"Yes Elton
Alifurai mno, Akaninyanyua taratibu mpaka kitandani. Usiku ule kwa mara ya tatu, tulipeana vizuri tu. Utamu mpaka kisogoni nawaambia na
uzuri ni kwamba Elton hata hakunikomoa kama siku ile nilivyo omba maji ya kunywa
Tulipotosheka tumekumbatiana zetu tukalala tukiwa
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi