*AFANDE NILEGEZEE KAMBA ππ«π«* *19&20* FINAL Kwa takribani masaa mawili tuliyatumia njiani mpaka kufika tulipokua tunaenda. Apo kwenye
masaa mawili kulikua na foleni plus kuna mda shangazi alitaka kujisaidia. Ila ayo masaa mawili kwangu yalikua kama dakika 101 Niliona kama tuliwai kufika mapema sana
Anyways, jumba lilikua ni jumba kweli! Wakwe zangu wanaonekana kuishi expensive life kushinda hata sisi. Kwa nje tuliona walifunga. maturubai ya kizungu alafu kulikua na shamra
shamra za kufa mtu
Yani wageni waliokua pale walishaanza kulewa. maana kama ni pombe zilikua za kumwaga ni wewe tu na kichwa chako.
Baba, Mama na Shangazi walikua wa kwanza. kushuka. Baba akakumbatiana na Rafiki yake pale huku wakiruka ruka kama watoto,
Nikaona mama nae anakumbatiana na Mke wa rafiki yake na baba ambae ni mama mkwe wangu mtarajiwa. But kuna kitu kilinishangaza, ni kwanini Mama mkwe anafanana sana na mama yake Elton?? Walifanana mno nikaishia kusema duniani wawili wawili bhana.
Ajabu ni kwamba hata yeye aliponiona pindi niliposhuka kwenye gari alinishangaa vile vile. Asiingeweza kunishangaa kama asingekua ananijua. Aliniangalia sana ila na yeye pia akadhani amenifananisha.
Basi tulikaribishwa kwanza ndani kwaajili ya utambulisho. Tulikaa sebuleni tukitazamana na familia ya Mume wangu.
Utambulisho ulifanyika, tulijitambulisha na wao.
wakajitambulisha. Sasa ndo ukaja mda wa kumtambulisha bwana harusi. Kwanza Mama wa bwana harusi akaomba radhi akidai Bwana harusi alichelewa kidogo maana ndo kwanza. amefika kwaiyo anamalizia kujiandaa
Tukiwa tunamsubiri bwana harusi tukapewa vinywaji vya kulainisha koo. Ila mimi akili yangu hata haikua pale, nilikua namuwaza Elton tu na huko alipo.
Baada ya dakika 15 Tukaambiwa Bwana harusi yupo tayari. Kwanza wakatoka ndugu zake wa kiume. Na Nilishangaa kumuona Elijah akiwa
miongoni mwa ndugu wa Bwana harusi. Hapo ndo nikahisi kuna kitu hakipo sawa kabisa.
Elijah mwenyewe alishtuka akabaki ananitazama kama kapigwa na radi. Si ndo Bwana Harusi akatoka bhana! Ni yeyeee.... Ni Elton huyu huyu Bwana Afande OCS!!
Sijui ilikuaje nikasimama bila kuelewa kama nimesimama Wageni na wazazi wote pale sebuleni wakanishangaa. Ule mshangao ukafanya Elton atizame upande wangu si akaniona bhana.
Bila aibu akaja mbio mbio kama mtoto alieona pipi, akanikumbatia kwa nguvu.
"Ginah! Unajua ni kiasi gani nimekutafuta????..... kwanini uliondoka???....."
"Sikua na namna Elton, sikutaka uogombane na mamaa yako kisΙ mimi"
"Nooo! Hukupaswa kuondoka Ginah! Kwanini hukuniamini!" Alilalamika na kuzidi kuwachanganya watu pale sebuleni
"Kwani unafanya nini hapa??"
" Na wewe unafanya nini hapa??" Akaniangalia kuanzia juu mpaka chini
"Oooh! wewe ndo bwana harusi???"
"Na wewe ndo Bwana harusi!" Alishangaa mpaka na pua
Nilichukla "kwalyo mimi nimeondoka kidogo. ukaamua kwenda kuoa mwanamke mwingine!"
"Na wewe umeamua kuondoka ili ukaolewe na mwanaume mwingine sio??"
"Unataka kusema mimi ndo mwanamke ambae wazazi wako walikua wanakulazimisha umuoe??"
"Ndiol Na hii inamaanisha kuwa mimi ndo mwanaume ambae wazazi wako walitaka uolewe nae!"
Tulishangaa, na watu wakazidi kutushangaa!
Ulikua ni mwendo wa kushangaana pale sebuleni. Ikabidi Mama Elton asimame na kuanza kusimulia maana yeyee angalau alikua anajua kilicho endelea.
Alipomaliza kuelezea akaja akanikumbatia na kuniomba msamaha maana hakupaswa kufanya alichokufanya hata kama hakutaka niolewe na mwanae.
"Nimejua kweli wewe ndie uliepangia kuwa na mwanangu! Karibu kwenye familia yetu Ginah
"Asante Mama" nilimkumbatia kwa furaha Elton akaona wivu. Akamsogeza mama yake pembeni kisha akanikumbatia yeye, akilalamika na kunieleza jinsi gani alivyo nimiss.
Watu walicheka na kufural na kushangilia sana. Ni Elijah pekee ndie alikua kimya. Ila alitufuata pia akidai kuna kitu alitaka kutuambia kwanza, alisema
"Sorry bro! Mimi ndie niliemwambia Mama yako kuwa unaishi na Ginah! Sio vizuri nilivyofanya lakini ni mapenzi tu yalinifanya nifanye ivi ila
nimejifunza kitu leo! Wewe na Ginah mlipangiwa
kuwa pamoja. Licha ya Ginah kutoroka
nyumbani kukimbia ndoa, still ulienda kukutana na kupendana na mwanaume ambae ulipaswa kuolewa nae! So am happy for you! Nawatakia all the best!"
"Usijali Bro! Pengine usingemwambia Mama tusingejua ukweli! Thanks!" Elton alishukuru
"And, nikisikia hata siku moja unamliza Ginah. nitakuja kukunyang'anya"
"Weeeeul lyo vita itakua sio ya nchi hiif Ila sidhani kama Ginah atawal kuja kulia kwa sababu yangul Atakua analia tu pale anapokata
kitunguu"
Wote tulicheka na kukumbatiana! Baada ya hapo tukahamia upande wa nje ambapo sasa zoezi la kuvalishana pete lilifuatia. Finally nikawa mchumba rasmi wa Bwana Elton Joshua.
Sikuamini ujue.
Then watu wakala, wakanywa na kuserebuka utadhani ndo ilikua mwisho wa dunia. Baadae jioni tulirudi nyumbani. Wazazi wangu walikua na furaha hata zile hasira zao juu yangu ziliisha.
kabisa
Wiki iliyofuata maandalizi ya harusi yakaanza. Hakuna kipindi nilichoka kama icho. Sijui
kuchagua gauni la harusi, mara viatu, mara nywele, mara kwenda kanisani kufundishwa ndoa! Huku Elton alitaka ale tamu yake jamani
nilihisi kuchanganyikiwa
Ila Hatimaye kila kitu kikaenda sawa na ndoa ikafungwa. Nikawa mke wa Elton halali kabisa. Baada ya ndoa tulirudi zetu Arusha mahali mapenzi yetu yalipoanzia.
Tulirudi nyumba ile ile tulikokaa kabla, lakini
sasa tulikua kama wake na mume. Mnajua Elton alinibadilisha sana?? Sikuwa nakunywa pombe, mambo ya club hakuna tena! Na kubwa zaidi Niliendelea na elimu yangu ya chuo kikuu nikafanikiwa kupata degree yangu ya kwanza.
Na kwakua Baba alikua amefungua tawi dogo la kampuni yake huku Arusha, akaniambia
nisimamie pale maana hakua na mtu mwingine anae muamini zaidi yangu. So maisha yamekua matamu kiasi hiko! Na-enjoy na mume wangu mbali ya kuwa sasa tuna watoto wawili ila ni
kama tulioana janal
Alafu eti hajawahi kunita baby! Bado ananiita tapeli eti anadai nilimtapeli moyo wake, ila jamani
-MWISHO-
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi