*AFANDE NILEGEZEE KAMBA ππ«π«* Chapter 8 Nilikumbuka jinsi chai inavyopikwa, nikadhani labda kahawa nayo ni hivyohivyo
Basi Elton alivyoshuka chini akakuta kikombe mezani cha kahawa akafurahi. Akaenda moja kwa moja mezani akaanza kunywa lakini ilipofika kwenye koo Alitema kisha akapiga kelele
"We tapeli! Njoo hapa haraka!"
Niliposikia tu ile sauti ya hasira, nikajua nimeharibu. Nikakimbia hadi dining, nikamkuta amekaa akiniangalia vibaya.
"Una akili kweli? Hivi ndio unavyopika black coffee?"
Sikusema kitu nilinyamaza
"Kwa nini umeweka sukari ndani? Na tena umeweka nyingi hivi?"
Sio uongo nilitia sukari nyingi maana huwa napenda sana vitu venye sukari sukari, nikadhani na yeye anapenda hivyohivyo, Kumbe hapana ndo niliharibu kabisa. Ikawa sio black coffee tena balli maji ya asali
"Am sorry, pole sikujua
Akanitazama kimya kwa sekunde chache, akavuta pumzi kama mtu anayejizuia asinirarue.
"Leo cousin wangu anakuja, Nataka upike chakula cha mchana. Anapenda mihogo ya nazi. Na pia utatengeneza mchuzi wa kuku, Umenielewa?"
Nikajibu "Ndiyo, nimekuelewa"
"Kama ukiharibu tena na mcharia, utajua kwanini watu huniogopal Akaondoka zake, kidogo Nilishusha pumzi kuwa Angalau hakunipa adhabu.
Majira ya mchana mchana Nikajitayarisha kupika. Nikaenda kwenye fridge nikachukua kuku na viungo, lla tatizo kubwa sikujua kupika chochote...
Najua mngesema ni google, lakini mimi sikuwa na bando wala hela ya kununua bando. Mtu pekee ambaye angeweza kunisaidia alikuwa mlinzi, lakini Elton alikuwa amemtuma mjini. Nikasema basi, sina namna ngoja nijaribu tu
Nikaosha kuku nikamuweka pembeni, nikakata nyanya, vitunguu na pilipili, nikaweka pamoja. Vyote nikavitia kwenye sufuria na maji ya kutosha. Apo kwenye maji ya kutosha nilitia maji kweli kweli.
Nikaacha vichemkie weee, vilipokaribia kuiva, nikaweka chumvi ila nilisahau kuonja kama ilikolea.
Baada ya hapo, nikaanza maandalizi ya mihogo
ya nazi. Nilikata mihogo kwa jinsi nilivyojua mimi, nikaosha kisha nikachemsha pamoja na nazi.
Ndani ya kama nusu saa kila kitu kilikuwa kimeiva.
Nikapanga mezani vizuri kabisa, kama vile wafanyakazi walivyokua wanaandaa meza nyumbani kwetu. Meza ilikuwa smart, chakula kinanukia vizuri. Nikaamini labda leo sitahaharibu chochote.
Saa nane hivi Elton akarudi na cousin wake. Nilivyowaona nikashangaa kumbe cousin si mwanamke, ni mwanaume. Jamaa anaitwa Elijah.
Duh, mzuri balaa. Alivaa smart, anatabasamu
mda wote na anaongea vizuri tofauti kabisa na kisirani Elton. Alipoingia ndani akanitazama, akatabasamu na kunisalimia. Ila Elton yeye alinipita tu kama hanioni viles.
Wakaingia sebuleni wakakaa kisha nikaagizwa nipeleke wine. Nikaenda jikoni ambako kuna kakabati kadogo ka wine. Ndani ya kabati kulikua na chupa moja ipo nusu tena ni wine pendwa ya Elton na ndiyo hiyo niliagizwa.
Bhana wee ile nimeshaitoa tu kabatini, sijui ilikuaje nikateleza niikadondosha ile chupa ya wine chini, paaaaah ikavunjika! Yani ule mlio wa chupa kuvunjika uliwafanya Elton na binamu yake wote waje jikoni spidi spidi.
Elton alifika wa kwanza akiwa na hasira.
"Hii ni nini sasa? We mikono yako haina nguvu? Kila kitu lazima uvuruge?"
Nikajibu kwa sauti ya woga "Sorry.......niliteleza tu, halkuwa makusudi"
"Kila dakika wewe ni makosa tu unafanyal Kila siku upuuzi mpyal We ni mwanamke wa aina gani? Lakini kwenye utapeli ndo wa kwanza"
Nikanyamaza tu, machozi yananilenga, ikabidi Elijah ajaribu kumtuliza
"Bro, achana naye. Ameomba msamaha. Ni ajali tu"
Elton akamjibu kwa hasira "We kaa mbali na huyu tapeli. Mimi ndo ninae mjua vizuri"
Elijah akasema kwa upole "Sawa, lakini usimkasirikie sana"
Elton akatulia kidogo kisha akaondoka zake. Elijah nae akamfuata sebuleni.
"Bro usichukie bhana"
"Its okay Elijah! Mda umeenda ngoja tule kwanza Alissema Elton akivuta akae huku Elijah akifungua hotpot
Ajabu ni kwamba Elijah alipofungua hotpot alianza kucheka vibaya mno. Elton akamuuliza, "Kwani nini kinachekesha?"
"Bro, hii lazima ulone mwenyewe!"
"Nini?" Elton akasimama kuangalia kwenye hotpot, alichokiona kilimfanya acheke kidogo badala ya kukasirika.
Mnajua nilivyopika ile mihogo Nilitia nazi nzima? Yani vile vile na vifuu vyake hata sikuvunja wala kukuna. Nikaacha zichemkie huko na ile mihago
Alafu kwenye hotpot ya kuku, ilikuwa kama supu ya maji, kuku anaelea juu juu kama anaogelea.
Elton akasema "Unaona sasa kwa nini mimi ni mkali kwake? Hii ndio kazi anafanya! Hebu fikiria ningekuwa nimeleta wageni muhimu leo, ningeumbuka namna gani? Lakini kabla sijaumbuka, lazima nimfundishe adabu!"
Je nini kitaendelea?
Nakuja
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi