Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MADAM NIPE KIDOGO BASI 15

10th Sep, 2025 Views 37


Basi bana maisha yakawa yanaendelea kwenda kama kawaida, na mume wangu aliendelea kunifanya kuwa mwanamke wa thamani na mwanamke bora sana kwake, hakuyumbishwa na maneno ya mtu yoyote Yule, maana yeye ndio aliamua kunipenda na hakuna mtu mwingine yoyote Yule ambae anaweza kuuvunja huo upendo ambao alikuwa nao kwangu…

Siku moja nilirudi nyumban mapema baada ya kupigiwa simu na mwalimu wa mwanangu kuwa mwanangu anaumwa, nilipofika nyumban, nikamkuta mama yangu mkwe, nikamkuta pamoja na kaka mmoja wa mume wangu, alikuwa mkubwa sana kwa mume wangu, inawezekana hata akawa marika yangu, ila alikuwa mlevi balaa, pamoja na yule binamu wa mume wangu…

Kitendo cha kuingia ndani tu nikapokelewa na maneno, sikutaka kubishana na mtu, nikaenda kumuangaia mwanangu na baada ya hapo nikaenda jikoni maana nilikuwa nasikia njaa sana, ila kabla sijala, nikasikia Yule dada wa mume wangu, ambae ni binamu anasema “ yaan kazi kula tu na kumloga kaka yangu, unajua gharama ya hicho chakula kweli wewe…

Sikutaka kumjibu, nikanyanyuka na kuanza kwenda zangu chumban kwangu, nikashangaa mtu kaja kukibweta chakula, alikuwa ni mama mkwe, kisha akasema “ hauna haki ya kula chakula ambacho amekitafuta mwanangu bibi kizee wewe, nikamuangalia bila kusema neno kisha nikataka kuondoka, nikashangaa naanza kupigwa, mama yangu mkwe akaanza kunifinya na Yule shemeji yaangu akaanza kunipiga mateke, nashangaa wananipiga ila sikuwa najua hata wananipigia nini, nikawa nalia, na watoto wangu wakawa wanakuja kuamua, na Yule ambae nilimzaa kabla ya kuolewa na Kendrick nae akawa anapigwa akaachwa mtoto wa Kendrick tu, aisee nilipigwa sana mpaka nikawa hoi, kisha mama mkwe akasema “ huo ndio mwanzo , ila nitahakikisha mpaka unaondoka kwneye hii nyumba, Yule ambae unamuona kama dada wa kazi, ndio anastahili kuwa mama mjengo wa nyumba ya mwanangu na sio wewe bibi kizee…

Sio siri nilijisikia vibaya sana kwakweli, nikaingia ndani, nikaanza kuoga, ila wakati natoka bafuni nikashangaa namuona mume wangu, akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ nani ambae amekufanyia hivi…

“ nilikutana na vibaka wakanipiga, nikajibu maana sikutaka kufarakanisha familia ya watu..
Kendrick akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akaenda kupiga ngumi ukutani, kisha akatoka nje, na kuongea kwa sauti ya ukali kuwa “ nani amemfanyia vile mke wangu…

“ mwanangu kwani mke wako amefanyiwa nini, itakuwa amepata laana za mungu baada ya kunitukana maana mimi ni sawa na mama yake, ila hana adabu anakaa na kuanza kunitukana, akawa anasema mama yangu huku akiwa anajifanhya analia, wakatyi huo mimi nilikuwa nafungasha virago vyangu, sikutaka kuendelea kukaa na watu kama wale, labda kama wataondpoka, mume wangu alijaribu kunizuia nisiondoke ila nilikataa kata kata maana sikutaka vita tena, na kwa namna ambavyo wananichukia wanaweza kunidhuru zaidi………

Nikaondoka zangu, na mume wangu alishindwa kunizuia ila akaondoka na mimi na kwenda kunilipia guest nzuri kwa ajili yangu na wanangu kisha akarudi nyumban kukaa na ndugu zake, ila anafika tu akashangaa anaanza kusikia mama yake anasema “ ila martin umejua kumchapa Yule mchawi, yaan nilitaman uchjukue chuma maana niliona kama fimbo haimuumi, maana kukaa na mchawi ni hatar sana, na Yule wakike akasema “ yaan nilikuwa nataman nimnyonge afilie mbali kabisa, na mama yake kendrickl akasema “ sio kumnyonga tu, ulitakiwa ujaribishe yule anaroho ngumu kama ya paka kwa maana asingekufa haraka…
Mara Kendrick akakohoa na kusema “ angalau paka amepata mume mwenye roho kama yap aka kama yeye…
Watu wote walitahamaki, maana hakuna hata mmoja ambae alihisi huenda Kendrick anaweza kuwa eneo lile…….

Mama yake Kendrick akaanza kujichekesha na kisema “ nimeshamuondoa huyo mchawi, nina uhakika utapata mwanamke bora..
ITAENDELEA……………

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MADAM NIPE KIDOGO BASI 15  >>> https://gonga94.com/semajambo/madam-nipe-kidogo-basi-15

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest