Kila mtu alimshangaa, maana alikuwa ni kijana mwenye nidhamu sana, hakuna mtu hata mmoja ambae angefikiria kuwa yale majibu yalikuwa yanatoka kwa Kendrick…
Kuna mwalimu alikuwa anaitwa Feisal alikuwa ananitaka, akataka sasa kwenda kummalizia hasira, ila mwalimu mmoja akaja akasema “ muacheni mimi nitaongea nae…
“ unajua kafanya nini huyu kijana, amemtongoza mwalimu, anatakiwa kuadhibiwa vikali sana, akasema mwalimu Feisal na wakati huo Kendrick hakuwa hata na wasiwasi kana kwamba anachokifanya ni sahihi sana…..
Yule mwalimu akamfata na kumuuliza ‘ unampenda sana madam si ndio..
Kendrick akawa kimya, walimu waliokuwa pale wakawa wanataka kimchapa. Ila Yule mwalimu alikuwa ni mwalimu wa nidhamu akawazuia, kisha akasema “ hawezi kupigwa, maana kila mtu ana haki ya kupenda, na anahaki ya kupendwa, huyu sio mtoto mdogo, na nina uhakika kabisa anajua ni nini anafanya, nina uhakika kabisa kuwa hisia za mapenzi nay eye anazo kama watu wengine, hivyo mimi nitaondoka nae, na sitaki kuona wala kusikia mtu yoyote Yule akimpiga huyu mtoto….
Kisha akamfata Kendrick na kuondoka nae, waliingia kwenye ofisi yake ya taaluma kisha wakaanza kuongea, waliongea sana, na sijui kwa kweli walikuwa wanaongea nini, ila waliongea kwa karibu lisaa lizima, na baada ya hapo Kendrick akatoka pekee yake, akaniangalia kwa dakika kadhaa kisha akatabasamu na kuondoka zake….
Kuanzia siku hio tabia zake zikabadilika, alikuwa anaishi kama mtu mzima sana, kimaamuzi na kivitendo kabisa, alikuwa hataki utani kabisa na maisha yake, akawa anasoma kwa juhudi kubwa sana, mpaka maendeleo yake yakaanza kurudi kuendelea kuwa ni miongoni mwa wanafunzi ambao wanafanya vizuri sana…
Maisha yakaenda, hakuwa ananisumbua tena, ila ikitokea nimeingia darasan alikuwa ananiangalia sana, nilikuwa nina uhakika kuwa hakuwa ananielewa kabisa, ila alikuwa anavuta taswira yangu mimi nay eye…
Sikujali nikawa napambania majukum yangu, maana sikutaka mazoea yoyote nae..
Ila sasa akaanza wivu, yaan akawa hatamani kuniona hata nikiongozana na mwalimu wa kiume au hata mwanafunzi wa kiume, yaan kwa wanafunzi alikuwa anaenda kumuanzishia vagi la maana, ila kwa walimu a alikuwa anatulia ila atafanya jambo lolote lile, ili kuhakikisha kuwa mimi na huyo mwanaume hatukai kwa utulivu…
Hapo sijui Yule mwalimu alimuambia nini Kendrick mpaka akawa hanisumbui, ila alikuwa hawezi kukaa bila kuniona, yaan kwa kuwa nilikuwa vijijini, alikua kila weekend anakuja kwangu kuomba kunichotea maji pamoja na wenzake, niliona kama jambo la kawaida sana…
Kumbe mwamba anatafuta namna nzuri ya kuonana na mimi kila wakati, nikajua kichaa chake kimeshapoa, maana sikuona usumbufu wake tena, kumbe alikuwa ametulizwa kwa muda na alikuwa amepewa maelekezo mengine kabisa, ambayo alikuwa ana uhakika kuwa mimi ni wake kwa namna yoyote ile…
Basi maisha yakawa yanaendelea, na kama mnavyojua mimi ni mwanamke na damu inachemka sana, hivyo nikawa nawaza kuingia kwenye ndoa sana, nilikuwa natamani sana kuolewa, au kuwa na mwanaume, ukilinganisha nilishawah kuingia kwenye ndoa, kuna namna hata mwili wangu ulikuwa unahitaji mwanaume wa kunikung’uta vumbi kidogo…
Basi kuna siku tulienda semina walimu wote, nikakutana na mwalimu mmoja, ambae ilikuwa kama utani tu tukazoeana, tukajikuta tunakuwa watu wa karibu sana yaan, tukawa tunawasiliana sana, tukajikuta tunaingia kwenye mahusiano…
ITAENDELEA……………
.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments