Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MIMBA YA DHARURA 15

12th Sep, 2025 Views 47



Misukosuko haikuishia kati ya kabir na jayden mara kwa mara walikuwa wakipishana kauli. Nadia akiona hali inaenda kuwa mbaya aliamua kuchukua maamuzi magumu .
Siku hiyo alitoka ofisini kwake akaenda ofisini kwa kabir.
" Karibu sana mwandani wa moyo wangu.
Nadia akiweka barua mezani kwa kabir.
" Boss hii ni barua yangu ya kuacha kazi.
Kabir alimuangalia usoni kwa makini kisha akachukua ile barua na kuisoma.
" Nini sababu ya wewe kuacha kazi?
" Nilijua mambo yanaenda sawa lakini naona kila siku zinavyoenda mambo yanazidi kuwa magumu kelele kati yako na jayden haziishii.

Kabir alimuangalia kisha akaichana ile barua na kutupia vipande vya karatasi kwenye dastbin.
" Naomba unipe muda wako , naomba jioni tukapata pamoja chakula cha usiku.
Nadia alimuangalia huku akiwa anajiambia.
" Sasa muda wa kumueleza ukweli umefika.
" Vipi unafikiria nini?
" Sasa nipo tayari .
" Asante kwa kukubali ombi langu.

Ilifika muda wa kutoka kazini Nadia alirudi kwanza nyumbani kwake kumuangalia mtoto wake .pia hakutaka kutoka akiwa kavalia mavazi ya kiofisi . Aliingia bafuni akaoga na kujiweka vizuri.
Alichukua gauni lake safi na zuri akavaa , alichukua pochi yake ndogo kisha akaondoka na kuelekea hotel ya Rose garden.
Alifika na kumkuta kabir ameshafika alikuwa akimsubiri.
" Pole kwa kuchelewa.
" Usijali .
Muhudumu alifika hadia aliagiza kinywani na chakula .
" Nimeitikia wito nakusikiliza boss wangu.
Wakati Nadia anaongea macho yake yalikuwa yakimkagua kabir jinsi alivyokuwa kapendeza . Kusema kweli kabir alikuwa ni bonge la mwanaume, anakipenda na kujijali. Yani ukimuangalia tu mwili wako unasisimka.
" Nadia nina mambo mengi ya kuongea na wewe kwanza kabisa naomba nikuombe msamaha kwa kile kilichotokea kipindi kile porini.
Nilitamani niongee kitu na wewe lakini hukunipa nafasi , kama ungenipa nafasi basi nisingepitia misukosuko niliyopitia na wala haya yote yasingetokea.
" Umepita misuko siko gani?
“Nadia… hujui nimepitia
Siku niliyoondoka pale hotelini nilihusi nimeacha kitu kikubwa sana huko nyuma.
Nilitamani kujua ulipo kuna muda nilienda dar nikikupa matumaini naweza kukuona lakini haikuwa rahisi nilikata tamaa na kurudi Arusha.
Yani kuna wakati nilihisi napagawa hakuwa chizi kwaajili yako Nadia
Ndugu zangu waliona kama nachanganyikiwa wakaamua kunilazimisha kuowa Ndio maana hata ndoa yangu haikuwa chaguo langu. Nilikaa nikijifariji labda ipo siku nitakutana na wewe.
Siku niliyokuona nilihisi mwili mzima kupata ganzi, kwanza sikuamini kama wewe ndio ipo kwenye sherehe yangu ya harusi. Nilikosea furaha mpaka mke wangu akajua sipo sawa.
Nadia leo hii umekaa mbele yangu, unanifanya niamini miujiza ipo.” sasa hebu niambie kuteseka kote huko leo hii nikuache uende kwa Jayden?

Maneno yale yalimgusa Nadia moja kwa moja moyoni. Hisia zilizokuwa zimefichwa kwa muda mrefu zikafufuka kama moto uliokuwa unataka kuzima alafu upepo ukaufufua tena. Machozi madogo yalimtoka bila hata yeye kujua.

Walijikuta wote wakinyamaza, wakitazamana tu kwa muda mrefu. Ndipo Kabir aliponyoosha mkono wake na kumgusa Nadia taratibu. Nadia hakujizuia, alijisogeza karibu zaidi na kabla hajajua walijikuta midomo yao imekutana na kupigana busu zito
Hawakujali tena muda wala sehemu, walijikuta wakihitaji faragha.
Kabir alisimama
" Nisubiri hapa nakuja .
Nadia aliitikia kwa kichwa
kabir alienda kuchukua chumba kwenye ileile hotel waliyokuwa wamekaa.
Baada ya muda kabir alirudi na kunyoosha mkono na Nadia alimpa mkono wake , walishikana mikono yao na kwenda kwenye chumba alichochukua
walijumuika pamoja kwenye ulimwengu wao wa mahaba. Safari hii Nadia hakuaogopa alikuwa huru sana na kabir alionekana kuwa na hisia nzito sana , sauti za mahaba na miguuni ulitawala ndani ya kile chumba.
Usiku mzima uligeuka kuwa wa hisia kali, Ilikuwa kama ndoto ambayo kila mmoja hakutaka aamke

Baada ya mapumziko kadhaa Nadia akawa amejipata juu ya kifua cha Kabir, moyo wake ulijaa wasiwasi na mchanganyiko wa furaha na . Alijua muda umefika. Hakutaka tena kuficha.

“Kabir…” alitamka kwa sauti ndogo
“Hmmm, my love…” Kabir alimjibu huku akipapasa nywele zake.
" Lakini wewe una mke ujue.
" Usijali kuhusu hilo mimi nitakua nini cha kufanya.
" Au unataka kunifanya mchepuko?
" Kamwe haitawezekana wewe ni nafasi yangu ya kwanza lazima nifanye halali.
" Unataka kumuowa mke wa pili?
" Ndio nadhani dini yangu inaruhusu.
" Vipi mkeo atakubali?
" Haitajalisha amekubali au amekataa nitaangalia msimamo wangu na uzuri anajua iuwa kuna mwanamke nampenda anaitwa Nadia.
Nadia hakuamini kwa haraka maneno ya kabir akimchukulia kama wanaume wengine na porojo zao.

Nadia akavuta pumzi ndefu.
“Kuna kitu muhimu sana nataka nikueleze. Naomba usinishangae, naomba usinihukumu ila ni lazima ujue.”
Kabir akatazama uso wake kwa makini. “Nadia, niambie. Hata iwe nini, nitakuelewa.”
" Nataka ujue mimi ni mama , nimezaa na nina mtoto wa kiume.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MIMBA YA DHARURA 15  >>> https://gonga94.com/semajambo/mimba-ya-dharura-15

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest