Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

MIMBA YA DHARURA 3

26th Aug, 2025 Views 19



Kabir alitamani kuongea kitu lakini Nadia alikuwa na hasira sana,
Amina rafiki yake Nadia alimuangalia sana kabir kama vile alikuwa anataka kuuliza kitu. Kabir aligundua hilo taratibu aliondoka kwenye lile eneo akaenda chumbani kwake.
" Nadia naomba usilie , hebu twende ukapumzike.
Amina alimshika mkono wakaenda chumbani
Nadia alisimama pembeni ya mlango wa chumba chake, moyo wake ukiwa bado na huzuni. Rafiki yake, Amina, aliiona uso wake uliokuwa umejaa huzuni na macho yaliyochoka.
" Nadia utakuwa na njaa nikakuletee chakula?
" Hapana sina njaa.
"Mbona unaonekana kuchoka na midomo imekaukia hata uso wako kama una huzuni , nini kimekupata huko ulikotoka?" Amina aliuliza kwa sauti ya hofu.

Nadia alifuta machozi yake kwa mkono, kisha akasema kwa sauti ya chini.
"Niโ€ฆ ni hofu tu ya kupotea Amina. Usijali, nilikuwa na hofu sana sikutegemea kama ingetokea salama kwenye pori la wanyama wakali"
Amina alijaribu kumkumbatia.
" Mungu ni mwema sasa upo salama Salmin ni jambo la kushukuru sana.
" Kweli. Nahitaji kupumzika.
Nadia alienda kupanda kitandani akachukua shuka na kujifunika mpaka usoni.

Wakati huo, Kabir alikuwa chumbani kwake, akijitazama kwenye kioo. Kila alivyokuwa akikumbuka kile kilichotokea, moyo wake ulima zaidi.
" Kwanini nimefanya vile kwanini sikujizuia? Nimemuuliza sana binti wa watu na sijui nawezaje kufuta jeraha nililompatia .
Kabir alijutia sana kwa maumivu aliyosababisha kwa Nadia.

Siku iliyofuata asubuhi na mapema Kabir aliuvaa ujasiri na kuamua kwenda kuonana na Nadia. Alifika kwenye mlango wa chumba akagonga . Mara amina alifungua mlango .
" Habari za asubuhi!
" Salama.
" Samahani Nadia ameacha amka?
" Ndio yupo macho.
" Samahani naomba uniitie nahitaji kuongea nae.
" Sawa.
Amina alifunga mlango akamfuata Nadia ambae alikuwa kakaa kitandani.
" Nadia kuna mgeni wako anataka kukuona.
" Ni nani?
" Yule kaka uliopitwa nae .
Nadia alikaa kimnya kwa muda baada ya sekunde alishuka kitandani akavaa viat.
Alifungua mlango na kumuona kabir akiwa kuegemea ukuta pia alikuwa amevaa vizuri alipendwa sana. Lakini Nadia hakujali muonekano wake alimuangalia huku akiwa kakunja sura.

"Habari, Nadiaโ€ฆ naweza kuzungumza nawe?" Kabir aliuliza kwa sauti ya unyonge.
Nadia aliangalia pembeni kisha akasema
"Samahani Kabir, siwezi, siwezi kuzungumza sasa. Tafadhali niache.
" Nipe muda kidogo wa kuongea na wewe ili moyo wangu uwe na amani kwani hata mimi najiona nina hatia najutia kwa kile kilichotokea , sikutegemea kufanya kile kitendo.....
" Inatosha kabir sasa naomba ufuate mambo yako na ukae mbali na mimi fanya kama hatujawahi kuonana. Nadia alimaliza kuongea kisha akaingia ndani na kuifunga mlango kwa nguvu mpaka Amina akashituka.
" Jamani hiyo ni mipango ya hotel sio ya nyumbani kwenu.

Kabir alihisi moyo wake ukivunjika, lakini hakupata njia nyingine. Kwa huzuni, aliondoka, akisogea polepole hadi chumbani kwake. Alikaaa kitandani akashuka kichwa chake . Baada ya sekunde alisimama akachukua kalamu na karatasi akaanza kuandika barua kwa Nadia. Aliandika kila neno kwa masikitiko, kuomba msamaha, na kuelezea jinsi anavyohisi maumivu yake kwa kile alichomfanyia.
Baada ya kumalizia, kuandika alitoka chumbani akampelekea Amina ile barua na kumuomba amfikishie Nadia.

Amina alienda chumbani akamkuta Nadia kasimama dirishani akiangalia nje.
" Nadia barua yako.
Nadia alishituka
" Barua? Inatoka wapi?
" Kwa yule handsome sombesombe.
Nadia lakini aliogopa kusoma aliweka barua kwenye begi lake bila kuisoma.
" Nadia kuna nini kinaendelea kati yako na yule kaka?
" Hakuna kitu.
" Au anakutongoza? Lakini mbona kama imemnunua vile kwani huko porini kimetokea nini? Amina aliuliza maswali mengi ilikutana kujua kilichojificha lakini Nadia hakufungua mdomo wake kujibu hata swali moja.

Siku hiyo hiyo, Kabir aliondoka hotelini akijua hatari na matokeo ya matendo yake yakiwa yameanza kutawala maisha yake yote sababu alihisi kudhurumu kitu kwenye maisha ya Nadia.
Ilipofika mchana Nadia alihisi kuwa na kosa kumuhukumu kabir kama kitendo walifanya wote na hakulazimishwa wala hakuweza kupinga.
Kwakuwa kesho walikuwa wanaondoka pale hotelini aliamua kwenda kuongea na kabir wasameheane tu.
Alipofika alikuta mlango wa chumba umefungwa alijaribu kugonga kujawa kimnya . Alipita muhudumu.
" Dada hicho chumba hakuna mtu.
" Yule kaka.....
" Kabir ameshaondoka asubuhi.
" Ameondoka?
" Ndio.
Baada ya kujibiwa hivyo Nadia akajikuta anajisikia vibaya na kujutia kwanini hakuna muda wazungumze
Aliondoka taratibu kuelekea chumbani kwa nia ya kwenda kuisoma ile barua aliyoandikiwa na kabir.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MIMBA YA DHARURA 3  >>> https://gonga94.com/semajambo/mimba-ya-dharura-3

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
profile
mjukuu 26 Aug 2025 18:57
MIMBA YA DHARURA 3
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest