MUNGU NISAMEHE NIMEMT*OA MIMBA BINTI YANGU! Mwaka 2008 ndiyo niliachana na mama wa mtoto wangu
Nilikaa kwa miaka kama 5 hivi. Kuna siku nikamkumbuka, nikaamua kumtafuta kwenye simu nikampigia, lakini simu yake ilikuwa haipatikani, hivyo nilijua labda amebadilisha namba na kama angekua na mtoto kweli ni lazima tu angenitafuta, sikuhangaika tena kumtafuta, nikaendelea na maisha yangu. Niliendelea na maisha, nikaoa na nina mtoto mwingine sasa.
Kuna siku rafiki yangu mmoja alinipigia simu, akaniambia kuwa kuna changamoto anapitia yeye na mke wake. Nilimsikiliza, akaniambia kuna binti wa kazi aliyekuja hapo kwake na kampa ujauzito, hivyo hajui ni kitu gani cha kufanya.
Aliniomba, kwa kuwa mimi ni daktari, nimsaidie ni vidonge gani ni rahisi kumt*olea huyo binti mimba kwani ni binti mdogo ana miaka 1*6, na anatoka kijiji kimoja na mke wake, hivyo kama asipomtoa mimba itakuwa aibu kwa familia yake. Basi nilimwambia kuwa hakuna shida, nikamuelekeza vidonge vya kunywa pamoja na utaratibu wa kila kitu. Kweli alifanya hivyo, nikamwambia asubiri ili aone kama mimba itatoka asimuondoe kwanza.
Kweli alisubiri na kama nilivyotabiri mimba haikutoka, hivyo tukaanza kuangaika lakini ikagoma. Baada ya kushindikana kutoa kwa njia ya vidonge, alimleta kwangu ili mimi nimtoe kama vile anajifungua, kwani ujauzito ulishafikisha miezi mitano na mke wake alishahisi kitu. Kilichokuwa kikimsaidia ni umbo la huyo binti, hivyo mimba ilionekana kama vile kanenepa na si mimba.
Alikuja kweli, nikafanikiwa kumtoa, lakini baada ya kukamilisha kila kitu, yule binti aliumwa sana mpaka ikalazimika kushirikisha familia yaani mke wake jamaa akakiri na kweli mke akawa hana namna akamhudumia yule binti. Nilikua naenda pale nyumbani kumhudumia yule binti, lakini wakati namhudumia ndipo nilianza kumuona tofauti. Alikuwa anafanana sana na ex wangu — yule mwanamke ambaye nilimuacha na ujauzito.
Katika kuongea na shemeji, akataja jina kamili la huyo binti. Jina ni la mama yangu, lakini jina la ukoo ni la yuleyule mwanamke ambaye nilimuacha na mimba. Nikawa na wasiwasi. Nilipoendelea kuongea na shemeji yangu, akaniambia kuwa huyo binti mama yake alishafariki muda mrefu na alikuwa analelewa na bibi yake! Mama yake alifariki wakati wa kujifungua, alijifungua salama lakini baada ya wiki akapata changamoto kurudishwa hospitalini hakupona tena.
Niliomba kuelekezwa ile familia nilifikia mpaka kule kijinini nikakutana na Bibi yake, nilipomuona hata sikuuliza mara mbili kwani niliwahi kumuona siku ya graduation na nina mpaka picha zake kwani ingawa hakunitambulisha kama mwanuame wake lakini tulipiga picha nyingi na yeye. Bibi hakua ananikumbuka, nilijisikia vibaya sana lakini niakwa sina namna ikabidi kujitambulisha na kulazimika kudanganya kwamba wakati naachana na binti yake sikujua kama ana mimba.
Niliomba kumchukua mtoto wangu na kuomba nimsomeshe kwani nina haki, bibi alikubali lakini mtoto alikataa, alinijibu tu kama wewe ndiyo Baba yangu mzazi ni bora nibaki tu hapa kijijini. Nilimbembeleza sana lakini aligoma, basi niakamua nimuache angalau afikirie vizuri, nilimuomba msamaha kwa kila kitu, lakini hakutaka kunisikiliza, nikaondoka na nakusema nimpe muda ila nakumbuka aliniambia wewe si mtu mzuri, ungekua mtu mzuri mama yangu angenipa jina lako, kampaka kadi ya kiliniki haina jina lako inamaana mama yangu alijua wewe si mtu mzuri.
Nilijisikia vibaya kwani kwa namna alivyokua anaongea ni kama alikua anajua kilichotokea mimi na Mama yake, hivyo kwa aibu nililazimika kusema ukweli, nilikiri mbele ya Bibi yake nikaenda kulia kwenye kab*uri la Mama yake, lakini nilipotaka kuondoka naye nimekusamehe lakini nimeridhika nitabaki na bibi. Sikua na namna Zaidi ya kuondoka, najua bado ana hasira ila naomba Mungu sana ili aniruhusu niwe sehemu ya maisha yake, bado mdogo sana na kapitia mengi kwakua sikuwahi kuwa baba yake.
NB: Asubuhi hii tunamalizia OFA ya kitabu cha “HAKUNA KUACHWA ACHWA” kama umechoka mahusiano ya kulia lia basi usiikose hii!
MWISHO
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi
Maoni